30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Rais Ufaransa aitisha kikao cha dharura na vyombo vya usalama

PARIS,UfaransaRAIS   Emmanuel Macron jana alilazimika kuitisha kikao cha dharura na vyombo vya usalama kutokana na  maandamano ya mamia ya watu yanayoendelea mjini hapa kupinga serikali.

Msemaji wa serikali alisema   huenda hali ya hatari ikatangazwa kudhibiti hali hiyo.

Mandamano hayo ya kupinga ushuru katika bidhaa  za mafuta  yamekuwa yakiongezeka tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ambako waandamanaji wanapinga kuongezeka gharama za maisha.

Wakati baadhi ya waandamanaji  wakiandamana kwa amani, wengine wamekuwa wakipambana na polisi huku wengine wakiweka kambi katika eneo la  kumbukumbu la Arc de Triomphe.

Mandamano hayo yameshuhudiwa pia katika eneo maarufu mjini  hapa,  Champ Elysees, na polisi wanaendelea  kutumia mabomu ya machozi  na maji ya kuwasha dhidi ya waandamanaji hao waliokuwa wakivuka vizuizi vya usalama katika barabara hiyo.

Maofisa wa polisi walisema jana kwamba zaidi ya watu 100 walikamatwa mwishoni mwawiki mjini hapa  na Shirika la Habari la Uingereza, Reuters, liliripoti kuwa askari sita na waandamanaji 14 walijeruhiwa.

Polisi walisema   baadhi ya waandamanaji walikusanya kuni na mabaki ya ujenzi karibu na eneo la kumbukumbu maarufu la Arc de Triomphe na kuwasha vitu hivyo moto.

Hiyo ni  mara ya tatu katika wiki kadhaa waandamanji kujitokeza kuonyesha kero yao na kutaka  kukoma  ongezeko la kodi hasa katika   petrol huku wakimtaka  Rais  Macron kusikiliza kero zao, kwa kuandamana mitaani.

Waziri Mkuu,  Edouard Philippe alisema  polisi 5,000 walikuwa wamepelekwa maeneo mbalimbali ya jiji hili  kuwadhibiti waandamanaji hao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,702FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles