26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Netanyahu akabiliwa na tuhuma za ufisadi

JERUSALEM, Israel



MAMLAKA za dola nchini hapa zimesema   zina ushahidi wa kutosha unaoonyesha Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu anahusika na vitendo vya rushwa na ufisadi ingawa yeye anakanusha akidai tuhuma hizo zinasambazwa na wapinzani wake wa siasa.

Polisi hao walisema jana kwamba  uchunguzi wao unaonyesha  Waziri Mkuu  Netanyahu alipokea rushwa   kuingilia kati  katika moja ya kesi ambazo zilikuwa zikiikabili kampuni kubwa ya mawasiliano ya Bezeq.

Polisi walisema   wana ushahidi huo ambao unaonyesha wazi    Netanyahu  na mkewe Sara, walipokea rushwa hiyo na kufuja fedha  hizo  kupindisha ukweli.

Katika madai hayo Netanyahu anashuhutumiwa kujichotea mamlioni ya dola katika kampuni hiyo ya  Bezeq  kuviziba mdomo vyombo vya habari vilivyokuwa vikiripoti kesi hiyo.

Washauri wake wawili waandamizi wamegeuka kuwa mashahidi  na wanasema wamezipa mamlaka ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwapo  vitendo hivyo.

Waandishi wa habari ambao hapo awali walifanya kazi katika tovuti ya Walla wamewahakikishia polisi kuwa walisumbuliwa  na kulazimishwa kuandika habari nzuri tu zinazomuhusu Netanyahu.

Hata hivyo Netanyahu anakanusha taarifa hizo akisema zilianza kusambaa hata uchunguzi bado haujaanza kufanyika.

Kutokana na taarifa hiyo ya polisi kumeibuka wito wa kumtaka  Netanyahu ajiuzulu.

“Waziri Mkuu hana tena sifa ya kuendelea kushikilia nafasi yake ni lazima ajiuzulu hata leo,” alisema  Tamar Zandberg, ambaye anaongoza Chama chenye mlengo wa kushoto cha Meretz. “Israel ni lazima iingie katika uchaguzi,”aliongeza kiongozi huyo.

Hiyo ni mara ya tatu kwa polisi  kutangaza mashitaka dhidi wa waziri mkuu  huku mkewe akiwa ameshashitakiwa katika kesi tofauti zinazohusiana na matumizi mabaya ya fedha za serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles