22.7 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS TRUMP ATEMBELEA WAATHIRIKA WA KIMBUNGA PUERTO RICO

Rais Donald Trump wa Marekani amekisifia kitengo cha dharula na wafanyakazi wake walioko Puerto Rico kwa jinsi walivyo itikia wito wa kukabiliana na kimbunga Maria, ambacho kiliikumba ardhi hiyo kwa takriban wiki ya pili sasa, kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu kumi na sita na kuharibu maelfu ya makaazi.

Katika ziara yake hiyo ya kwanza tangu dhoruba hiyo ilipotokea, Trump katika mazungumzo yake juu ya gharama ya kurejesha maisha upya amesema kwamba watawasaidia kupitia bajeti ya serikali yake.

Hata hivyo, wakaazi walio wengi bado wana hasira kwa serikali yao kwa namna wanavyoshughulikia suala hilo.

Zaidi ya asilimia tisini na nane ya watu hawana nishati ya umeme na walio wengi zaidi hawana maji safi na salama ya kunywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles