23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

PROFESA MBARAWA: SERIKALI HAIKURUPUKI KUNUNUA NDEGE

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa leo amepangua hoja wa wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo huku akithibitsha kuwa Serikali inatarajia kununua ndege nyingine kubwa ya saba ya masafa marefu.

Amesema Serikali haikurupuki kununua ndege hizo kwa kuwa inao mpango kazi unaobadilishwa kila mara kulingana na wakati.

“Serikali itaendelea kununua ndege na haitakodi kwa sababu kukodi ni gharama kubwa ikilinganishwa na kununua.

“Nia ya serikali ni nzuri kwani huwezi kuwa na viwanja vya ndege kama huna shirika lako ndege hivyo tumenunua ndege sita ambazo tatu zimetua na zinafanya kazi. Mwaka huu tunategemea ndege tatu zitawasilisha ambazo ni Boeng 787 ya masafa marefu yenye uwezo wa kuchukua abiria 262, nyingine mbili zenye uwezo wa kuchukua abiria 132 kila moja ni Bombardier CHCS 300 ambazo zitawasilia na kuanza kufanya kazi.

“Kikawaida huwezi kuwa na ndege moja ya masafa marefu ikafanya kazi vizuri hivyo kwenye bajeti hii tumeshapanga kununua ndege nyingine boeng 787 ili tuwe na ndege mbili za masafa marefu ambapo moja ikiwa inatoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou na moja inatoka Guangzhou kuja Dar es Salaam. Ndio utaratibu unavyokwenda,” amesema.

Aidha, amesema kwamba Kampuni ya Ndege (ATCL), inao mpango kazi hivyo si kweli kwamba haina kama wabunge walivyodai ambapo kila baada ya muda inabadilishwa kwani si msahafu hivyo itabadilishwa kutokana na mahitaji ya soko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles