24.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 30, 2023

Contact us: [email protected]

TAKUKURU YASHINDA KESI SABA LINDI

Na Hadija Omary, Lindi

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Lindi, imeshinda kesi saba kati ya tisa walizozifikisha mahakamani katika kipindi cha Julai mwaka juzi hadi Machi mwaka huu.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Steven Chami amesema hayo leo Aprili 25, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Lindi.

Chami amesema katika kipindi cha miezi tisa taasisi hiyo ilipokea malalamiko ya wananchi yapatayo 104 kupitia njia mbali mbali zikiwemo kipindi cha longa nasi, televisheni, Radio, barua na magazeti.

“Kupitia malalamiko hayo taasisi imefanikiwa kuchunguza na kukamilisha majalada ya uchunguzi 11 na kuyawasilisha kwa Mkurugenzi Mkuu lakini pia tulifungua kesi tisa na kufanikiwa kushinda saba na kushindwa kesi mbili na kesi nyingine 16 zinaendelea,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Chami amesema kuwa miongoni mwa kesi hizo tisa zilizofunguliwa nyingi zilikuwa ni kutoka idara ya afya zikifuatiwa na zile za vyama vya ushirika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,203FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles