Prezzo, Jaguar wafikia pabaya

0
733

prezzoNAIROBI, KENYA

WASANII wa muziki nchini Kenya, Jackson Makini ‘CMB Prezzo’ na Jaguar, wamefikia pabaya baada ya wawili hao kurushiana maneno kupitia mitandao ya kijamii.

Awali Jaguar alimrushia maneno msanii huyo kutokana na kitendo cha utovu wa nidhamu ambacho alikionesha wakati anahojiwa na runinga ya Taifa. Jaguar alidai kwamba ‘umefika wakati Prezzo atafutiwe chuo kwa ajili ya kwenda kujifunza nidhamu.’

Kutokana na kauli hiyo, Prezzo ameshindwa kuvumilia hisia zake na kuanza kumshambulia msanii huyo ambaye ana mgogoro naye kwa kipindi kirefu.

“Niko tayari kwenda kwenye chuo ambacho kitanifanya niwe na nidhamu, lakini lazima Jaguar aanze yeye kwanza kwenda kujifunza Kiingereza vizuri kwa kuwa hajui kitu na akiongea hauwezi kumuelewa hata kidogo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here