Celine Dion apata pigo lingine

0
850

The Grammy Nominations Concert Live - ShowLAS VEGAS, MAREKANI

NGULI wa muziki nchini Marekani, Celine Dion, amepata pigo lingine la kufiwa na kaka yake, Daniel, ikiwa ni siku mbili tangu afiwe na mume wake, Rene Angelil.

Celine mwaka umeanza vibaya ambapo kabla ya kutulia na machungu na kufiwa na mume wake, anapata pigo la kuondokewa na kaka huyo ambaye alikuwa na umri wa miaka 59 ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani.

Daniel alikuwa anasumbuliwa na saratani ya ubongo na ulimi, kaka huyo alifariki mikononi mwa mama yake mzazi ambaye ana umri wa miaka 88, Therese.

Hata hivyo, kwa sasa Celine hajui la kufanya na wapi aanzie, lakini familia yake imemtaka kushughulikia kifo cha mume wake, huku familia hiyo ikifanya mpango wa kushughulikia mazishi ya mtoto wao, Daniel mjini Vegas.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here