24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAWAONYA WANAFUNZI KUHUSU CHIPS, LIFT

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA


DAWATI la jinsia na watoto mkoani Arusha, limewataka wanafunzi wa shule za msingi mkoani hapa kuwa makini na kujiepusha na mambo yanayoweza kuharibu maisha yao.

Wito huo umetolewa juzi na Mkuu wa Kitengo cha Dawati hilo ambaye pia ni Mkaguzi wa Polisi, Happyness Temu, alipokuwa akitoa elimu ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi 63 wa elimu maalumu katika Shule ya Msingi Meru mjini hapa.

Akizungumzia elimu hiyo, Temu alisema ilililenga katika vipengele vya ubakaji, ulawiti na vipigo kwa wanafunzi kwa kuwa baadhi yao hujikuta wakifanyiwa vitendo vya ukatili baada ya ushawishi wa kupewa lift na kununuliwa vyakula zikiwamo chipsi.

“Kununuliwa vyakula zikiwamo chips na lift za magari na pikipiki, vimekuwa vikisababisha ushawishi na hatimaye wanafunzi kufanyiwa ukatili wa kubakwa au kulawitiwa.

“Si wote wana nia mbaya pindi wanapotoa lift au kununua chakula. Ukweli ni kwamba, wapo wachache wenye nia nzuri na wengine wana nia ovu.

“Kwa hiyo, wazazi wanatakiwa kufuatilia kwa karibu na kuwaeleza uhalisia wa mabadiliko ya maisha watoto ili kuwaepusha dhidi ya wenye nia mbaya,” alisema Temu.

Kwa upande wao, Mwalimu Veila Wilson na John Maukiri wanaotafsiri kwa lugha ya alama, walisema baadhi ya wanafunzi wamefurahia elimu hiyo na kusisitiza kuwa itawasaidia kupata ufahamu wa hatua wanazoweza kuchukua katika kujiepusha na vitendo vya ukatili.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mussa Luambano, alilishukuru Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia na watoto kwa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wake.

Alisema kwamba, elimu hiyo itawasaidia wanafunzi wa shule hiyo yenye mchanganyiko wa wanafunzi wa elimu ya kawaida na elimu maalumu wakati wa kukabiliana na uhalifu dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles