30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

CCM YAREKEBISHA KATIBA YAKE

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimefanya marekebisho ya katiba na kanuni za chama pamoja na jumuiya zake baada ya kufanya mabadiliko makubwa ikiwamo kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamati na Halmashauri Kuu ndani ya chama hicho.

Marekebisho hayo ambayo yatapitishwa rasmi katika mkutano maalumu utakaoongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli utafanyika Machi 12, mwaka huu mkoani Dodoma, yametokana na uamuzi wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, iliyofanyika Desemba mwaka jana jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo imesema mkutano huo pia utapokea taarifa ya ratiba ya uchaguzi mkuu wa chama hicho na jumuiya zake utakaofanyika nchi nzima baadaye mwaka huu.

“Mkutano mkuu huu pia utatanguliwa na mikutano ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Machi 10, na wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Machi 11, mwaka huu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles