27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Polisi wapiga ‘stop’ mkutano wa Zitto Kigoma

Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi wilayani Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa madai ya sababu za kiusalama.

Mkutano huo wa Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, ulipangwa kufanyika leo Ijumaa Januari 17, katika Viwanja vya Mwanga Center, Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kwa mujibu wa barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma, Raphael Mayunga kwa Ofisi ya Mbunge huyo, Jeshi la Polisi limezuia mkutano huo kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizopo.

“Napenda kukujulisha kuwa mkutano huo umezuiliwa kwa tarehe uliyoomba kwa sababu za kiusalama kutokana na kiitelijensia zilizopo. Kwa hiyo huruhusiwi kufanya mkutano wala kuendelea na maandalizi ya mkutano huo.

“Aidha rejea Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi sura ya 322 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 katika Kifungu 43 (3) (4) (6),” imesema barua hiyo.

Akizungumzia uamuzi huo wa jeshi la polisi, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma, ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema; “sababu iliyotajwa bila shaka haina mashiko na inalenga kumzuia Zitto Kabwe kutekeleza shughuli zake halali za kutumikia wananchi wa jimbo lake.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles