Washington, Marekani
Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amekaribisha hatua za dakika za mwisho za kundi la Maseneta kupinga kuidhinishwa kwa ushindi wa uchaguzi wa urais wa, Joe Biden.
Maseneta 11 wa Republican na Maseneta wateule, wakiongozwa na Ted Cruz, wanataka kura ya kuidhinisha ushindi wa Biden kuchelewasha kwa siku 10 ili kuchunguza madai ya wizi wa kura.
Hatua hiyo huenda isifaulu kwa sababu Maseneta wengi wanatarajiwa kupiga kura ya kumuidhinisha Biden bungeni Jumatano Januari 6. Biden, ambaye ni Mwanachama wa Democratic, ataapishwa rasmi kuwa rais wa Marekani Januari 20.