26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Ummy atimiza ahadi, achangia mifuko 600 ya saruji Tanga

Amina Omari, Tanga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu amekabidhi mifuko 600 ya saruji yenye thamani ya sh Mil 8.4 kwa ajili ya kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari Jijini Tanga

Hafla ya makabiziano ilifanyika jana Januri 2, mbele ya Mstahiki Meya wa Jiji hilo, Mkurugenzi Mtendaji pamoja na watendaji mbalimbali wa Halimashauri hiyo.

Amesema wakati wa ziara yake hivi karibuni aliahidi kupeleka mifuko ya saruji katika shule tano kati ya kumi ambazo zinaendelea na ujenzi ili kuongeza kasi ya ujenzi lakini kusaidia kukamilisha kwa wakati ujenzi huo ili ifikapo Januari 11, wanafunzi wote waliofaulu waweze kuanza kidato cha kwanza.

“Nimevutika na jitihada ambazo Tanga Jiji mmeweza kuzifanya za kuusimamia ujenzi wa madarasa kwa nguvu kubwa hivyo nimeona niwaunge mkono ili muweze kukamilisha kwa wakati na wanafunzi wetu waweze kuanza masomo katika muda muafa,” alisema Waziri Ummy.

Aidha, amewataka wakuu wa shule na kamati zake kuzingatia miongozo ya Serikali katika kuwachangisha fedha wazazi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya elimu ya vijana wao ili kusiwepo na malalamiko wala manunguniko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles