29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Pellegrini amtabiria makubwa Guardiola

Pep GuardiolaMANCHESTER, ENGLAND

KOCHA wa Manchester City, Manuel Pellegrini, amedai kwamba klabu hiyo inaweza kufanya vizuri zaidi kama watafanikiwa kumchukua kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola.

Hata hivyo, kocha huyo amesema kuwa bado ana nafasi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mkataba wake utakapomalizika mwaka 2017 japokuwa kuna uvumi wa Guardiola kutua hapo Januari mwakani.

Guardiola amekuwa akiwindwa na klabu nyingi za Ligi Kuu nchini England, lakini Man City wanaonekana kuwa katika hatua za mwisho kumalizana na kocha huyo ambaye ana uhusiano wa karibu na viongozi wa klabu hiyo, Txiki Begiristain na Ferran Soriano ambao waliwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Barcelona.

Pellegrini anaamini kuwa kama Man City ina mpango kwa sasa wa kumchukua Guardiola basi atakuwa wa kwanza kupewa taarifa kutoka kwa viongozi wake.

“Ninaamini ipo siku Guardiola ataweza kuchukua nafasi katika klabu hii, nitafurahi sana kwa kuwa ataipa mafanikio makubwa, ila siwezi kumzungumzia zaidi kwa kuwa mimi sio yeye ila kocha bora lazima aje kwenye klabu bora,” alisema Pellegrini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles