Arsenal kumkosa Welbeck hadi Februari mwakani

0
745

WelbeckLONDON, ENGLAND

KLABU ya Arsenal inatarajia kumkosa mshambuliaji wake, Danny Welbeck, hadi Februari mwakani kutokana na kuwa majeruhi.

Kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger, amethibitisha kuwa staa huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda huo kutokana na majeruhi yanayomsumbua.

Kuumia kwa Welbeck kunaongeza idadi ya majeruhi katika klabu hiyo ambapo ataungana na Alexis Sanchez na Jack Wilshere.

Kutokana na hali hiyo, Wenger atakuwa katika wakati mgumu katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi.

“Kwa bahati mbaya Welbeck alikuwa majeruhi tangu Aprili mwaka huu na sasa ameumia tena ikiwa ni mwishoni mwa Desemba na bado ataendelea kutocheza kwasababu amevunjika mfupa.

“Jambo hili ni la kusikitisha na ni pigo kubwa kwetu kwa sababu siwezi kubadili timu,” alisema Wenger.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here