22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mashabiki Chelsea wamlilia Mourinho

MashabikiLONDON, ENGLAND

MASHABIKI wa Chelsea wameshindwa kuzuia hisia zao juzi katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Sunderland ambapo klabu yao ilishinda mabao 3-1, lakini walionekana wakiwa na mabango ambayo yanaonesha bado wanamuhitaji.

Kocha huyo amefukuzwa na klabu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini katika mchezo wa juzi mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, walionekana wakiimba nyimbo za kumsapoti Mourinho.

Kuna baadhi ya mashabiki ambao walionekana wakiwa na mabango ambayo yalisomeka ‘wewe ndio kocha wetu’.

Hata hivyo, kuna mashabiki walionekana kuwazomea nyota wa klabu hiyo, Diego Costa na Cesc Fabregas, wakidaiwa kwamba wamesababisha kocha huyo kufukuzwa.

Nafasi ya kocha huyo imechukuliwa na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Guus Hiddink, huku uongozi ukiamini kwamba kocha huyo atawapa mafanikio.

Hiddink baada ya kusaini mkataba na klabu hiyo, amedai kwamba amerudi Chelsea kwa lengo la kurudisha heshima ya klabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles