23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Panya sasa kutumia uzazi wa mpango

Grey rat on a white background close up

NA MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

CHUO Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kimepata suluhisho la kupunguza kuzaliana  panya nchini, kwa kuanzisha uzazi wa mpango kwa wanyama hao.

Akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana, Mtaalamu wa Kilimo wa Chuo hicho, Thoneson Mhamphi alisema, utafiti huo ambao upo katika hatua za awali  haujaweza kusambazwa.

Mhamphi alisema dawa hizo za uzazi wa mpango zinazojulikana kama Quinestro na Levonorgester, zimekuwa zikichanganywa kwenye chakula na kuwapatia panya hao, hatua  inayowafanya washindwe kuzaliana.

“Huu utafiti ndiyo tumeanza kuufanyia kazi hivi sasa na   umeonyesha mafanikio kwa sababu  baada ya kuwapa chakula hicho panya hao wameacha kuzaana,” alisema.

Alisema dawa hiyo husababisha panya dume kuwa na nguvu ndogo ya kuzalisha kwa vile kizazi cha jike hujaa maji.

Mtaalamu huyo alisema panya wana  kasi ya kuzaliana ana anaweza kuzaa kila baada ya wiki tatu.

Vilevile, panya ana uwezo wa kupata mimba  tena  saa 24 baada ya kuzaa, alisema mtaalamu huyo.

Alisema   utafiti huo   unaendelea kufanyika katika hatua nyingine   kuona jinsi ya kukabiliana na panya waliopo   mashambani.

“Mlipuko wa panya ni mkubwa  na kama tusipopata njia za kuwadhibiti, hali katika mashamba yetu inaweza kuwa mbaya kabisa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles