33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

VILLAGE NATURISTE-CAP D’AGDE ‘Mji mkuu’ wa wapenda kukaa utupu duniani

UTUPU

NI mji mdogo lakini wenye mambo makubwa ulio katika pwani ya Bahari ya Mediteranian nchini Ufaransa ukiitwa Village Naturiste- Cap d’Agde.

Ukiwa katika pwani hiyo katika Mkoa wa Languedoc-Roussillon, umetokea kuwa moja ya pepo kubwa kabisa za maraha katika pwani ya Mediteranian ya Ufaransa.

Umaarufu wake duniani unatokana na kuwa ‘mji mkuu’ wa wapenda kukaa utupu duniani, ukivuta watalii wasioona soni ya kukaa utupu kutoka kona zote za dunia.

Unapoingia katika mji huo ni lazima uvue nguo na kuvinjari mtupu popote pale unapokwenda ikiwamo katika maduka ya kisasa, posta, saluni, benki na kadhalika.

Kwa sababu hiyo wakazi wake kwa mwaka mzima huishi wakiwa watupu na wakati wa majira ya joto wakazi huongezeka kufikia 40,000 kutokana na mmiminiko wa watalii.

Lakini imekuwaje mji huo mdogo wa Ufaransa ugeuke kuwa mji mkuu wa watupu duniani?

Nyuma miaka ya 1950 Ufaransa ilikuwa ndiyo inaponea majeraha ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na ilihitaji liwazo la kimwili na kiakili.

Hivyo, wakati familia moja ya wakulima wa zaituni mjini Cap d’Agde ilipotembelea ardhi yao ilipigwa na butwaa kukuta imejaa watu waliovalia vichupi pamoja na waogeleaji walio watupu na hivyo nao wakakijiunga na familia hizo.

Baada ya kupata kibali rasmi kinachohalalisha utupu katika ardhi yao hiyo katika miaka ya 1960, Klabu yao ya Oltra ikawa maarufu kama eneo kwa familia za watu wapendao uasili na kukaa utupu kutoka Ujerumani na Uholanzi.

Wakati baadhi ya watu waendao likizo walipojenga nyumba karibu na eneo hilo na kuanza kuishi eneo hilo kipindi chote cha mwaka, mji mzima ukawazunguka.

Wakati huo huo kile kilichoanza kama kituo kidogo cha posta kilichobatizwa kama ‘Ujerumani’ kikakua kuwa ofisi ya kwanza ya posta duniani ambayo watu wanaingia watupu.

Ufukwe wa Village Naturiste- Cap d' Agde
Ufukwe wa Village Naturiste- Cap d’ Agde

Kufikia miaka ya 1970, Serikali ya Ufaransa ikaangalia njia ya kuuendeleza ufukwe huo ambao awali lilikuwa eneo masikini zaidi nchini humo.

Wakati nchi nyingi zikitengeneza fedha kutokana na utalii, ni Ufaransa pekee iliyokuja na wazo la kutoza kodi ya kukaa mtupu.

Wageni katika mji huo hulipa pauni euro nane sawa na Sh 18,000 wafikapo getini, ambako huvua nguo na kuziweka katika loka.

Pia kumejengwa benki, saloni, maduka ya kisasa, migahawa, hoteli na mengineyo ambako unaingia ukiwa mtupu.

Wakati fukwe za utupu zikiwa zipo katika nchi nyingine, Cap d’Agde ni mahali pekee duniani ambako kuna maeneo hayo tajwa unaingia mtupu.

Leo hii wasafiri kama Collin Lee Erickson kutoka Ontario, Canada kuja kupata wanaoona uhuru wa asili wa kubaki mtupu, ambao huwezi kuupata popote nchini mwao.

“Ilikuwa safari yangu ya kwanza nje ya Amerika ya Kusini na nimepeta uzoefu mzuri pamoja na kufurahia maisha kwa namna ambayo haijawahi kunitokea,” Collin aliiambia tovuti ya news.com.au.

Badala ya kuvaa vichupi kama fukwe nyingine za utupu katika maeneo mengi duniani, katika ufukwe wa Cap d’Agde’ kukaa mtupu ni lazima.

Hata hivyo, tabia yoyote mbovu au chafu utakayokutwa ukiifanya hadharani inaweza kukupeleka jela sambamba na faini ya dola za Marekani 22,000 sawa na Sh milioni 44.

Jioni inapoingia mji mzima unakuwa na adabu kwa kujisitiri kwa ajili ya chakula cha usiku kwa vile mikao katika viti ni rahisi mno kuonesha kila kitu nyeti, kitu ambacho hakuna mtu angependa kuonekana hadharani.

Wakati usiku unapoingia familia huelekea kulala huku mitaa ya Cap d’Agde’ ikiingia katia migogoro na utata, hasa miaka ya karibuni.

Collin anaamini kuwa katika nchi nyingine fukwe zimelenga kutamanisha kingono tofauti na mji huu wa Ufaransa lakini kuna watu waliouharibu tofauti na malengo ya waasisi.

Wakati mji ulipoanzishwa na waasisi wake, haukulenga kuhusisha masuala ya ngono bali kuishi mithili ya simulizi ya vitabu vitakatifu ya Adamu na Eva katika bustani ya Aden kabla hawajatenda ile dhambi.

Hata hivyo, kwa sasa umekuwa sumaku wa watu wenye malengo ya kutongozana.

Na haikuwa ajabu wakati kiwanja kwa ajili ya familia maalumu kwa mapumziko kilichokuwa na bwawa la kuogelea kilipofyekwa na tingatinga mwaka 2005 ili kutoa fursa ya ujenzi wa baa na vilabu vya usiku ikiwamo vile ambavuo ni maalumu kwa wenzi na vya kubadilishana wake.

“Kutokana na mazingira haya mapya, Collin ambaye ni mpenda uasili anasema tabia zinazotokea ni za kitoto na si aina ambayo angezipenda.”

Hilo limeleta uhasama katika mji huo baina ya watu wanaopenda uasili na wale wenye kuendekeza ngono.

Kilele cha mivutano baina ya pande hizo mbili kilishuhudia Cap d’Agde’s “boite echangiste” (klabu ya usiku ya kupeana wake) ikiteketezwa kwa moto na mamlaka zilijitoa kusaidia ufukwe huo.

“Wapenda uasili wakalalamikiwa kusababisha moto huo ijapokuwa kesi hiyo hadi sasa bado haijatatuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles