24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Waanza kutafiti siri ya maisha marefu

Old-ManWilliam Shao,

Wakati wastani wa umri wa kuishi wa watu duniani ni miaka 71.4, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Duniani (mwaka 2015) yenye jina ‘Global Health Observatory’ katika eneo moja la Sardinia—ambalo ni kisiwa kikubwa katika Bahari ya Mediterranean—idadi kubwa ya wakazi wake wanaishi maisha marefu kupita umri wa miaka 100.

Sababu za wao kuishi maisha marefu kadiri hiyo hazijulikani kwa sasa, lakini hivi karibuni wanasayansi wanaweza kupata baadhi ya majibu ya maswali wanayojiuliza.

Kampuni ya Uingereza ya teknolojia ya mimea imenunua data maumbile (genetic data) za zaidi ya wakazi 13,000 wa jimbo la Ogliastra la Sardinia, Italia, kwa matumaini ya kupata siri ya maisha marefu.

Tiziana Life Science, ambayo ni taasisi ya kansa na kinga ya magonjwa yenye makao yake makuu mjini London, Uingereza, amenunua sampuli za kibiolojia za wakazi wa eneo hilo ili kujenga kile wanachokiita ‘benki ya kibaiolojia ya data’.

katika jimbo hilo, mmoja kati ya kila watu 2,000 huishi kuvuka umri wa miaka 100. “Hii ni mara tano zaidi ya nchi zilizoendelea kama Uingereza na Marekani,” likasema gazeti ‘Daily Mail’ la Uingereza.

Sampuli zilizochukuliwa zililinganishwa na taarifa za tiba za wahusika na kumbukumbu rasmi kama hati za vifo kwa zaidi ya miaka 400 iliyopita.

Tafiti za awali zilionesha kuwa watu wa baadhi ya maeneo kama Japani na Mediterranean waliishi maisha marefu zaidi kwa sababu ya kula samaki, matunda, mbogamboga na vyakula vyenye mafuta machache.

Hata hivyo, baadhi ya wanasayansi wananza kuipinga nadharia hiyo, na sasa wanaanza kuchunguza jamii zenye watu wanaoishi maisha marefu zaidi ili waone kama kuna sababu nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles