23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

PALESTINA YAZITAKA AMERIKA KUSINI KUTOHAMISHIA BALOZI YERUSALEM


CARACAS, VENEZUERA   |

RAIS wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ametoa mwito kwa nchi za Amerika ya Kusini kutounga mkono uamuzi wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wake mjini Yerusalem.

Akizungumza mjini hapa juzi katika mkutano uliohudhuriwa na Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Abbas amesema ana matumaini nchi nyingi za Amerika Kusini hazitahamishia balozi zake Yerusalem kwa vile hatua hiyo ni kinyume cha sheria ya kimataifa.

Kiongozi huyo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alimshukuru mshirika wake, Rais Maduro kwa kukataa kuunga mkono uamuzi wa Marekani wa kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem.

Kwa upande wake Maduro alisema anaunga mkono msimamo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na kuwa serikali yake inataka kutambuliwa kwa dola la Wapalestina.

Guatemala tayari ilitangaza kuhamishia ubalozi wake mjini Yerusalem siku mbili tu baada ya Marekani kutangaza hivyo.

Wakati hayo yakiendelea Paraguay imesema itahamishia ubalozi wake Jerusalem na kufuata hatua iliyochukuliwa na Marekani pamoja na Guatemala, kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Paraguay pamoja na wizara ya mambo ya nje ya Israel.

Aidha Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel Emmanuel Nahshon amesema katika taarifa yake kuwa Rais wa Paraguay, Horacio Cartes anapanga kuzuru Israel mwishoni mwa mwezi huu kufungua ubalozi wa nchi hiyo mjini Yerusalem.

Uamuzi huo wa Paraguay unakuja wiki moja kabla ya Marekani kufungua ubalozi wake wa Yerusalem Mei 14 kufuatia hatua ya Rais Donald Trump kutangaza hivyo Desemba 6 mwaka jana.

Uamuzi huo wa Trump ulipokewa kwa shangwe kubwa na Israel na kuwakasirisha Wapalestina.

Israel inasisitiza kuwa Yerusalem ni mji wake wa milele na usiogawanyika wakati Wapalestina wanataka eneo la mashariki wa mji huo liwe mji mkuu wa taifa hilo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles