24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MALEMA: BUNGE LA AFRIKA LIWE NA MENO KUDHIBITI SERIKALI AFRIKA


JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI   |

KIONGOZI wa Chama cha Wapigania Uhuru wa Kiuchumi (EFF) cha hapa, Julius Malema ametoa mwito wa kulipatia Bunge la Afrika (PAP) mamlaka kamili la kudhibiti mataifa ya Afrika.

Kwa sababu hiyo, ameitaka nchi yake kuongoza kampeni za kulipatia Bunge hilo mamlaka kamili ya kisheria ili chombo hicho kifanye kazi kwa ufanisi na manufaa ya watu wa Afrika.

Malema, ambaye aliapishwa kuwa mbunge wa PAP mjini hapa juzi, alisema Bunge hilo haliwezi kubakia kama chombo cha ushauri.

“Lazima liwe na mamlaka kamili kisheria, liwe na uwezo wa kuzichukulia nchi hatua. Mataifa mengi ya Afrika hayafuati misingi ya demokrasia, hayaheshimu matokeo ya kisiasa. Ufisadi umehalalishwa na nyendo nyingine zisizokubalika katika mataifa mengine mengi,” Malema alisema.

PAP ambacho ni chombo cha kutunga sheria cha Umoja wa Afrikan (AU) kina wajumbe 250 wanaowakilisha mataifa 50 wanachama wa AU, ambao walisaini itifaki ya kukianzisha. Kila taifa mwanachama huwakilishwa na wajumbe watano.

Mamlaka ya sasa ya PAP yamejikita zaidi katika kushauri na wakati huo huo kuwa jukwaa la watu kutoka mataifa yote ya Afrika kushiriki katika mijadala na utoaji maamuzi kuhusu matatizo na changamoto zinazolikabili bara hili.

“Lakini PAP haiwezi kuingilia kati kwa sababu halina meno. Nina furaha kuwa Bunge la Afrika Kusini limechukua uamuzi wa kutuma uongozi wake wa juu katika chombo hiki ili wasaidie kubadili mtazamo.”

“Lakini pia kutoa mbinyo kwa Bunge letu kusaini Itifaki ya Malabo, ili tuweze kusonga mbele na kuzihamasisha nchi nyingine kusaini itifaki itakayokipatia chiombo meno ya kuuma,” alisema Malema.

Itifaki ya Malabo inatoa mamlaka kwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACJHR), ambayo bado kuanzishwa, kushughulikia kesi za kimataifa za jinai na uhalifu chini ya sheria za kimataifa.

Itifaki hiyo ilipitishwa katika mkutanio wa wakuu wa nchi za AU na serikali Juni 2014, ambao ulifanyika mjini Malabo, Guinea ya Ikweta.

Nchi wanachama wa AU wametakiwa kusaini, lakini hadi sasa zilizosaini ni pamoja na Chad, Benin, Congo-Brazzaville, Ghana, Guinea-Bissau, Kenya, Mauritania, Sao Tome and Principe na Sierra Leone.

Mwanasiasa huyo mtatanishi wa Afrika Kusini pia alisema atapigania uwapo wa wanawake na vijana zaidi kutoka nchi wanachama.

Kwa sasa itifaki inasema wajumbe watano wa kila nchi wanachama angalau mwanamke awe mmoja.

“Tunatakiwa kuwa na asilimia 50 ya uwakilishi wa wanawake na kuwe na adhabu kwa mataifa ambayo hayatafuata mpangilio huo bila kuwasahau vijana,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles