23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

OPERESHENI YA KUKAMATA VIROBA YASHIKA KASI

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


SERIKALI imeendelea na operesheni  ya kukagua pombe zinazofungashwa  kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) ambapo jana katika Manispaa za Temeke na Kinondoni wamefunga  viwanda vya maghala kutoendelea na uzalishaji, kuuza wala kusambaza.

Kwa upande wa Temeke kiwanda cha Global Distillers Limited watengenezaji  wa pombe kali aina ya viroba aina ya Premium Vodka na Ginja ambapo walifanikiwa kukamata katoni 1500 na ghala ambalo lilikutwa na katoni 650.

Kwa upande wa Wilaya ya Kinondoni  na Ubungo kiwanda cha Kibo Spirit na True Bell navyo vilizuiwa uzalishaji baada ya kukuta pombe hiyo ya viroba ikiwa imesheheni aina ya Kitoko na Rivella Vodka kimakosa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo kwa upande wa Wilaya Kinondoni  na Ubungo  Mwanasheria wa Baraza la Mazingira (NEMC ), Heche Suguta,  alisema hilo ni zoezi endelevu lengo ni kuhakikisha agizo laserikali linatekelezeka kwa wafanyabiashara hao.

Alisema wanafunga na kusitisha uzalishaji huo hadi hapo utaratibu mwingine utakapofuatwa ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia mpya.

Alisema lengo ni kusimamisha uzalishaji na hata uingizwaji kwa kuwa vileo vingine vinatoka nje ya nchi.

Aliongeza kuwa hata kwa wale wa mpakani tayari wameshawasiliana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazuia uingizwaji na kama mtu amekamatwa basi anatakiwa mzigo wake urudishwe ulipotoka.

Katika manispaa ya Kinondoni pia ukaguzi ulifanyika katika maghala mbalimbali ikiwemo la Triple S Investment Company Ltd na muhusika kukimbia ambapo timu ya ukaguzi ilikuta makufuli yakiwa yamefunguliwa na jengo zima kutokuwa na mtu.

Katika ghala hilo pia ambalo muhusika alikimbia walikutana na vifungashio kwa nje aina ya Signal true Vodka ujazo asilimia 100.

Katika ghala la Kibo Sprit uongozi wa hapo walisema hawajaanza uzalishaji zaidi ya kuwa na ghala hilo.

Kwa upande wa Temeke , Kiongozi wa msafara katika timu hiyo  Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Aron Nzalla alisema ukaguzi wameufanya kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles