28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

MWANASHERIA MKUU WA MAREKANI MATATANI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump ameingia katika msukosuko mwingine wa kisiasa baada ya kubainika kuwa Mwanasheria Mkuu, Jeff Sessions, alifanya mazungumzo na Urusi wakati wa kampeni.

Mawasiliano hayo yameibua wito bungeni kumtaka ajiuzulu kufuatia uchunguzi unaoendelea chini ya Wizara ya Sheria.

Wizara hiyo inachunguza madai kuwa Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani uliomwingiza madarakani Rais Trump.

Sessions, ambae ni muungaji mkono wa mwanzo kabisa wa Rais Trump na mshauri wake wa kisera wakati wa kampeni, hakuweka wazi kile alichozungumza na Balozi wa Urusi, Sergei Kislyak wakati shauri hilo liliposikilizwa  mwezi uliopita.

Badala yake alidai hakufanya mawasiliano yoyote na Warusi.

Juzi usiku, Msemaji wa Wizara ya Sheria, Sarah Isgur Flores, alisema kwa hakika hakuna kilichopotoshwa katika majibu yake hayo.

Lakini taarifa hiyo, haikuwafurahisha wabunge wa Democratic, ambao kabla ya siku hiyo walishinikiza kiongozi huyo ajiondoe katika wadhifa huo ili asivuruge uchunguzi.

Kiongozi wa Chama cha Democratic katika Bunge la Marekani, Nancy Pelosi, amemtuhumu Sessions kudanganya licha ya kula kiapo na akamtaka ajiuzulu.

Wana Democratic wengine wamepiga kelele za kutaka ajiweke kando na uchunguzi huo kwa vile ni mtuhumiwa.

Katika taarifa yake, Sessions alisema hajawahi kukutana na ofisa yeyote wa Urusi kujadili suala la kampeni.

Lakini kitengo cha uchunguzi kimethibitisha kuwa akiwa Seneta wa Marekani na mjumbe mwandamizi wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Silaha, alifanya zaidi ya majadiliano 25 mwaka jana na Warusi.

Moja katika mikutano hiyo ilifanyika Septemba 2016 akiwa seneta, sambamba na mikutano mingine na wajumbe wa Uingereza, China, Ujerumani na mataifa mengine. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles