27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

WATU 600 WAPIMWA DAWA ZA KULEVYA

Na ESTHER MNYIKA-DAR ES SALAAM


MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samuel Manyele amesema sampuli za watu wanaotumia dawa za kulevya zimeongezeka kwa kipindi cha miezi miwili hadi kufikia 644.

Kutokana na hali hiyo na vita ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya nchini, wanatarajia hadi kufikia Desemba mwaka huu watapokea kesi 3,600 kwa ajili ya kupima sampuli za watu wanaohisiwa kutumia dawa hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Manyele alisema kesi za watu hao zilifikishwa katika ofisi yake kwa kipindi cha Januari na Februari mwaka huu ikiwa ni tofauti na mwaka 2015 ambapo walipokea kesi 1000 tu kwa kipindi hicho.

Alitoa takwimu hivi karibuni Mkuu wa Mkuu wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitaja watu wanaotuhumiwa kujihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya  ambapo katika orodha hiyo aliwataja wasanii, wanasiasa, viongozi wa dini pamoja na wafanyabiashara.

Kutokana na hali hiyoalisema Serikali  imenunua mtambo wa kisasa wa kupima sampuli tofauti unaoitwa ‘Energy Dispersive X-Ray Flourescence SPectrometer' (EDXRF) ambao umegharimu Sh milioni 101.7.    

Alisema kutokana  ongezeko la kupima sampuli za dawa za kulevya  ofisi hiyo imekuwa ikilazimika kusitisha kupima  sampuli zingine kwa lengo la kuwahisha  majibu ya watuhumiwa wanaoshikiliwa na vyombo  vya usalama ili hatua  za kisheria  zichukuliwa.

“Kesi za madawa ya kulevya zimeongezeka katika kipindi cha miezi miwili  ya Januari na Februari tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Profesa Manyele.    

Alisema Ofisi ya Mkemia imeanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya kupokea kesi za dawa za kulevya tu ili kurahisha majibu ya kesi hizo kupatikana kwa wakati na kufanyia  matengenezo  mitambo husika.

 Alisema waliweka mtandao maalumu kwa ajili ya kusafilisha sampuli za dawa za kulevya zinazotoka mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.     

Alisema mwaka 2015 walichunguza sampuli mbalimbali 60,000 mwaka 2016 sampuli 120,000 na mwaka huu wanatarajia kuchunguza milioni moja katika uchunguzi huo na gharama zitaongezeka.

“Kutokana na wingi wa kesi walilazimika kwenda kwa Mpiga Chapa wa Serikali ili kupata karatasi za siri ili kuepuka kuvuja kwa majibu hayo na  wafanyakazi kulipa malipo ya ziada kwa sababu walikuwa wanafanya kazi saa 18 na  kuhakikisha majibu yanapatikana kwa wakati ,”alisema  Profesa Manyele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles