26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

ONYANGO ATABIRIWA MAKUBWA AFCON

LIBREVILLE, GABON


MLINDA mlango wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Joseph Bell, amemtabiria makubwa mlinda mlango wa timu ya taifa ya Uganda, Dennis Onyango, kuwa atang’ara katika michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika nchini Gabon.

Mkongwe huyo wa soka amedai kuwa, kipa huyo kutoka nchini Uganda amekuwa na mchango mkubwa katika klabu yake ya Mamelodi Sundowns ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini, hivyo kuna uwezekano wa kufanya makubwa zaidi nchini Gabon.

Bell aliwahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mara mbili pamoja na kufanya makubwa katika Ligi Kuu nchini Ufaransa wakati anakipiga katika klabu ya Marseille, anaamini kipa huyo kutoka nchini Uganda ana uwezo mkubwa.

“Kuna wachezaji wa kuwatazama katika michuano hii ambao wataleta kivutio kikubwa, wapo wachezaji wa ndani lakini wapo walinda milango ambao wanapewa nafasi kubwa, kwa upande wangu ninaamini kipa kutoka nchini Uganda, Dennis Onyango, ana nafasi kubwa ya kusumbua kwenye michuano hii.

“Mlinda mlango mwingine ambaye ninampa nafasi ya kufanya vizuri ni pamoja na Essam El-Hadary ambaye anaiwakilisha timu ya taifa ya Misri, wachezaji hao kwa upande wa walinda milango wana nafasi kubwa ya kufanya makubwa sana kwa michuano hii,” alisema Bell.

Hata hivyo, nyota huyo ameongeza kwa kusema kuwa hakuna timu ambayo itafanya vizuri katika michuano hiyo bila ya kuwa na mlinda mlango mwenye uwezo mkubwa, hivyo walinda milango wana nafasi ya kuifikisha timu yao mbali.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles