30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Nyota Simba waungana kumuombea Inonga abebe kombe AFCON

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Wachezaji wa Simba wameungana na mchezaji mwenzao Henock Inonga kumuombea aweze kufika fainali ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) hata kubeba ubingwa wa michuano hiyo inayoendelea nchini Ivory Coast.

Inonga ambaye ni beki wa Simba anaitumikia timu ya Taifa ya DR Congo ambayo keshokutwa Februari 7, 2024 itashuka dimbani kucheza na wenyeweji Ivory Coast katika mchezo wa nusu fainali.

Beki wa Wekundu wa Msimbazi hao, Hussein Kazi ndiye aliyeweka bayana kuwa wachezaji wa Simba wanamuombea mwenzao aweze kufika mbali na kuchukua ubingwa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

“Sisi kama Simba wachezaji kwa ujumla, tunamuombea mwenzetu Inonga mazuri aweze kufika mbali na kuchukua kombe,” amesema Kazi wakati akizungumzia maandalizi kuelekea mechi yao na Tabora United, utakaochezwa kesho Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mkoni Tabora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles