30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MNEC Gungu atoa vitabu vya Uongozi na Maadili

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika kuadhimisha miaka 47, ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, Taifa (MNEC), Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Gungu, ametoa vitabu vya uongozi na Maadili ya Chama, Katiba na Kanuni kwenye Kata zote za Mkoa huo, ili kuwawezesha Viongozi ambao wanataka kuomba uongozi ndani ya Chama kujua kazi zao.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Kata ya Nyaluwande, wilayani Busega, Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, amesema vitendea kazi hivyo kwa viongozi hao ngazi ya Kata vitawasaidia kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa na kukisaidia chama kutekeleza majukumu yake vizuri.

“Kama mtakumbuka vizuri mwaka jana tukiwa Maswa wakati tunasherekea sherehe kama hizi niliahidi kutoa vitabu hivi kwa Mkoa mzima, leo navikabidhi hapa tukiwa tunasherekea miaka 47 ya kuzaliwa CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Emmanuel Gungu Silanga akimkabidhi vitabu vya kanuni za uongozi na maadili Mwenyekiti wa CCM Simiyu Shemsa Mohamed Seif katika maadhimisho ya miaka 47 ya sherehe za kuzaliwa chama hicho wilayani busega mkoani simiyu

“Vitendea kazi hivi ni nyenzo nzuri kwa viongozi wetu kuweza kutimiza majukumu yao vizuri. Hii pia itawasaidia hata wale ambao wanataka kuwania nafasi za uongozi ndani ya chama kujua kazi zao,” amesema Gungu.

Kutokana na hatua ya Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoa vitabu hivyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed Seif amepongeza kwa kueleza kuwa vitabu hivyo ni msaada mkubwa kwa Chama, kwani vitasaidia kuwajenga viongozi na kuwawezesha kujua majukumu yao.

“Naomba nikupongeze sana MNECc Gungu, umefanya jambo kubwa sana vitabu hivi vitawasaidia viongozi wetu kuwaimarisha na kuwajenga vizuri kutekeleza majukumu yao naomba nichukue nafasi hii kukupongeza sana,”alisema Shemsa.

Gungu pia katika maadhimisho hayo alitoa mifuko ya saruji 30 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Kata ya CCM Nyaluwande sambamba na kutekeleza ahadi yake ya kutoa mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi ya Zahanati ya Kata ya Shigala Wilayani Busega, ambapo wananchi wa kata hiyo walimuomba kutokana na Kata hiyo kukosa Zahanati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles