30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Nyati azua taharuki wilayani Nkasi

Gurian Adolf- Nkasi

WAKAZI  wa Kijiji cha Kate wilayani Nkasi mkoani Rukwa, wamekumbwa na  taharuki kubwa, baada ya mnyama aina ya nyati kuvamia kijiji hicho na kusababisha wananchi kushindwa kuendelea kwenye shughuli zao.

Akizungumzia tukio hilo jana,  Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo,Philbert Kwimba alisema nyati huyo alianza kuonekana tangu juzi kijijini hapo, hali iliyosababisha wananchi kushindwa kutoka nje ya makazi yao  kuhofia usalama wao.

Ofisa Tarafa wa ya Kate, Bazilio Mazungwa alisema nyati alikutwa nyumbani kwa mfugaji mmoja kijijini hapo juzi  saa moja asubuhi, hali iyosababisha wananchi kushindwa kutoka nje ya makazi yao kwa kuogopa  kukutana naye.

Alisema  kutokana na hali hiyo, walitoa taarifa mamlaka husika ya Serikali kwa lengo la kuomba msaada ili wananchi wa waweze kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Alisema  hadi sasa hakuna taarifa zozote mbaya zilizoripotiwa tangu  nyati huyo kuvamia katika kijiji hicho na wananchi wameendelea kuchukua tahadhari.

Kaimu Ofisa Maliasili na Utalii wa Wilaya ya Nkasi,Frank Wakungwa alisema idara yake kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori TAWA wamekwenda eneo la tukio kukabiliana na nyati huyo ili kuondoa hofu inayowakabili wakazi  hao.

Alisema kuna namna mbili ya kufanya, kwanza ni kumrejesha nyati huyo ndani ya hifadhi ya Lwafwi alikotoka au kumuua kama ataonekana  ni hatarishi kwa usalama wa wananchi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,873FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles