23.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

Ayatollah Khamenei atoa miongozo kuhusu Palestina

MWANDISHI WETU

KIONGOZI Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei, ametoa miongozo saba muhimu kuhusu jinsi ya kuendeleza Jihadi kubwa na takatifu.

Kiongozi huyo alisema hayo mwishoni mwa wiki katika hotuba yake ya Siku ya Kimataifa ya Palestina ambapo alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuanza awamu mpya ya mapambano ya Palestina baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.”

Alisema Mwongozo wa asili kabisa ni kuendeleza mapambano na kupanua wigo wa Jihadi katika ardhi zote za Palestina na kwamba kuainisha Siku ya Palestina ni ubunifu wenye busara wa Imam Khomeini ambao uliwaunganisha Waislamu ili wawe na sauti moja kwa ajili ya Palestina tukufu.

Ayatullah Khamenei, alitoa miongozo saba muhimu aliyotoa kwa watu wote wanaofuatilia sana masuala ya Palestina ambapo miongoni mwa miongozo hiyo ni kutobanwa maudhui ya Palestina katika masuala ya Kipalestina au Kiarabu tu.

Mwingine lengo la mapambano haya ni kukomboa ardhi yote ya Palestina kuanzia Mto hadi Bahari na kurejea Wapalestina wote katika ardhi yao.

Alisema hayo yatapunguza malengo hayo kwa kutosheka na suala la kuundwa dola katika sehemu ndogo ya ardhi hiyo si alama ya kupigania haki wala si kielelezo cha kutilia maanani ukweli wa mambo, kwa sababu hii leo mamilioni ya Wapalestina wemefikia upeo wa juu wa fikra na kujiamini kiasi kwamba, wanaweza kusimamia mapambano hayo ya Jihadi na kuwa na matumaini ya nusra ya Mwenyezi Mungu na ushindi wa mwisho.

Katika mwongozo mwingine ametilia mkazo ulazima wa jamii ya Waislamu wenye ghera na wanaoshikamana na mafundisho ya dini kutawakali kwa Mwenyezi Mungu katika Jihadi hii kubwa na takatifu na kutegemea nguvu zao za ndani na kujiepusha kuyategemea madola ya kidhalimu ya Magharibi, jumuiya tegemezi za kimataifa na baadhi ya nchi vibaraka na zisizo na heshima za kanda hii ya Asia magharibi

Mwongozo muhimu zaidi wa Ayatullah Khamenei, ni mwongozo wake wa sita ambapo ametaka ‘kudumishwa kwa mapambano na kuenezwa uwanja wa jihadi katika ardhi zote za Palestina.’

Huku akisisitiza kuwa watu wote wanapaswa kulisaidia taifa la Palestina katika jihadi hiyo takatifu, na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inajivunia kutangaza kwamba itatekeleza wajibu wake katika uwanja huo kadiri ya uwezo wake.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kwamba, mabadiliko hayo yatabadilisha uwiano wa nguvu katika ardhi zinanazokaliwa kwa mabavu na kuifanya Palestina ikaribie hatua ya kuanzisha hujuma, na kwamba Mamlaka ya Ndani ya Palestina ina wajibu mkubwa katika uwanja huo.

Katika mwongozo wake wa mwisho Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa Palestina ni ya Wapalestina wote na kwamba inapaswa kuendeshwa kwa matakwa yao.

Alisema kuchomoza Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran kulifungua awamu mpya katika mapambano ya Palestina.

“Medani ya mapambano ni hatari sana, yenye mabadiliko na inayohitajia kuwa macho daima. uzembe na makosa katika mahesabu muhimu katika mpambano huu muhimu sana na unaoainisha mustakbali wa Umma, vitasababisha hasara kubwa,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,293FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles