NONDO ATETA NA WAKILI WAKE

0
716

NA GABRIEL MUSHI - Dar es Salaam

HATIMAYE Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Abdul Nondo, amefanikiwa kuzungumza na mmoja wa mawakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC).

Pia imebainika tangu aokotwe Mafinga mkoani Iringa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi ni siku ya 16 (hadi Machi 22, mwaka huu) hajawahi kuoga wala kubadilisha nguo alizovaa.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, alisema kwa mujibu wa wakili aliyetumwa kwenda kuonana na Nondo, ilibainika nguo alizovaa ni zilezile tangu wasamaria wema wamvalishe baada ya kumwokota.

“Ni kweli wakili wetu alienda Iringa Alhamisi wiki hii na kuongea naye, nguo ni zilezile tangu wasamaria wema wamvalishe baada ya kumwokota.

“Kuongea anaongea vizuri ila kwa muda mchache ambao wakili wetu alipewa kuongea naye, anasema akili yake haipo sawa, lakini hajaonyesha kama amepigwa popote.

“Katika mazingira hayo ni dhahiri kuwa hajaoga kwa sababu …

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here