29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

FATMA KARUME AKOLEZA JOTO UCHAGUZI TLS


Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

UAMUZI wa Wakili Fatma Karume kujitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), unatazamwa kuamsha joto la uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Aprili 14.

Tayari jina la Fatma limeishapitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho, sasa anasubiri kufunguliwa pazia la kuanza kampeni ya kutafuta ushawishi kwa wanachama wenzake.

Si Fatma pekee aliyepitishwa na kamati ya uchaguzi kuwania urais, bali yapo majina mengine matatu ya mawakili nguli ambayo yameingia katika kinyang’anyiro hicho.

Mawakili hao ni Godwin Ngwilimi ambaye kwa sasa ni makamu rais wa chama hicho, Godwin Mwapongo na Godfrey Wasonga.

Fatma ambaye pia ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, akifahamika kwa misimamo isiyoyumba, pia si mkimya pale panapofaa kuuzungumzia ukweli.

Hulka yake hiyo ndiyo iliyoamsha joto kutokana na kuingiza jina lake katika kinyang’anyiro hicho wakati ambao TLS imemlalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuchomeka vipengele viwili, kikiwamo kile kinachoweka masharti magumu dhidi ya sifa za mgombea wa urais wa chama hicho.

Hilo linaweza kuthibitishwa na namna ambavyo jina lake limekuwa likijadiliwa sana na wanasheria wenyewe, lakini pia katika mitandao mbalimbali ya kijamii mara tu baada ya kutangaza kuwania nafasi hiyo.

Katika mijadala hiyo, baadhi ya watu wamekwenda mbali na hata kukumbuka misimamo ya Fatma katika suala la Katiba Mpya, utawala wa sheria na haki, lakini pia jinsi ambavyo alifika mahakamani kumtetea Rais wa sasa wa TLS, Tundu Lissu katika kesi ya uchochezi inayomkabili.

Pamoja na kwamba jicho la watu wengi ni kwamba Fatma anapewa nafasi ya kushinda uchaguzi huo, hata hivyo duru za mambo kutoka katika mifumo ya chama hicho, zinadai atakumbana na ushindani mkubwa kutoka kwa wagombea wengine, hususani Ngwilimi.

Pia wagombea wengine kama Wasonga na Mwampongo nao si wa kupuuzwa katika kinyang’anyiro hicho kutokana na uzoefu wao ndani ya taaluma ya sheria.

Wakati uchaguzi huo ukiwa mbioni kufanyika, hali ya sintofahamu imetanda miongoni mwa wanachama kutokana na kanuni mpya ya …

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles