22.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 5, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yakabidhi milioni 15 udhamini wa mashindano ya Makisatu

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Benki ya NMB imekabidhi Sh milioni 15 kwa ajili ya udhamini ya mashindano Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (Makisatu) yaliyofunguliwa rasmi  jana Jijini Dodoma .

Akizungumza jana Mhazini Mkuu wa Beniki ya NMB, Azizi Chacha alisema benki hiyo imetoa fedha hizo ikiwa ni udhamini wa mashindano hayo yanayondaliwa na Serikali kupitia wizaaara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ambayo yalizinduliwa rasmi jana Jijini hapa.

Chacha alibainisha kuwa lengo la NMB  kusaidia fedha hizo  ni kuisaidia Serikali katika kufanikisha mashindano hayo ya Kitaifa ambayo yamekuwa na malengo ya kuibua wabunifu wapya kila mwaka .

Alisema  NMB  inashiriki katika mashindano hayo kwa kuwa ni wadhamini na wamekuwa wakiwasaidia baadhi ya wabunifu katika kufanikisha ndoto zao za kuendeleza ubunifu huo kwa kuwapa mikopo .

Alibainisha kuwa kuna baadhi ya wabunifu wamekuwa na miradi ambayo inaajiri watu wengine hivyo wakiwezeshwa watatoa ajira zaidi kwa vijana na makundi mengine.

Kadhalika alisema NMB imekuwa ikishirikiana  na Serikali katika mashindano hayo kila mwaka ili kuhakikisha wabunifu wapya wanaibuliwa kila mwaka kwa lengo la kulisidia taifa

Aidha alisema NMB inamilikiwa na serikali kwa asilimia 38 hivyo ni jukumu la benki kuiunga mkono serikali katika kuwezesha miradi na mipango mizuri ilikusudiwa .

Aliongeza kuwa NMB imekuwa ikisaidia Jamii katika maeneo mbalimbali ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Hata hivyo alisema NMB imekuwa ikitoa misaada mbalimbali katika shule za msingi na sekondari kwa kutoa madawati,meza na viti kwa ajili ya shule wanafunzi kutumia  wakati wa masomo .

Kwa upande wake Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako  aliwashukuru Benki ya NMB na wadau wengine  kwa kuwaunga mkono katika mashindano hayo kwa kutoa kiasi hicho cha fedha .

Prof.Ndalichako  aliwaomba NMB kuendelea kudhamini mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kwa washiriki kufanya maonesho kwa wiki moja.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutenga bajeti zaidi ili kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa lengo la kuibua wabunifu wapya kila kona ya nchi

Alisema mashindano hayo yanashirikisha wabunifu kutoka vyuo vya ufundi,shule za msingi ,Vyuo vikuu na wabunifu binafsi kutoka maeneo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles