‘Nitangoja’ ya Janet Otieno yafika patamu

0
364

NAIROBI, KENYA

MWIMBAJI nyota wa gospo nchini Kenya, Janet Otieno, amewashukuru wapenzi wa muziki huo kwa kuipokea vyema video ya wimbo wake mpya, Nitangoja uliotoka hivi karibuni.

Akizungumza hivi karibuni jijini Nairobi hivi karibuni, Janet alisema ujumbe wa wimbo huo unaosisitiza watu kuwa na subira pale wanapongoja baraka za Mungu, umefikia hatua nzuri kwenye mitandao ya kijamii na chati mbalimbali za muziki ndani na nje ya Kenya.

“Watu wengi wanasema kupitia wimbo wangu Mungu ameongea na watu kuhusu subira. Hii ni hatua kubwa kwenye huduma yangu ya uimbaji na ninaendelea kusisitiza kwamba muda mwingine tunakuwa kuwa na subiri tunapongoja baraka za Mungu, video tayari ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube,” alisema mwimbaji huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here