26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Shibuda agoma kwenda kupiga kura

Derick Milton, Simiyu

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADA-TADEA, John Shibuda amegoma kwenda kupiga kura hadi pale mawakala wake katika majimbo ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi mkoani Simiyu watakaporuhusiwa kuingia katika vituo vya kupiga kura.

Shibuda amesema kuwa hawezi kwenda kupiga kura endapo mawakala wake hawataruhusiwa kuingia katika vyumba hivyo baada ya kuzuiliwa kwa kile kilichoelezwa kuwa hawana barua za utambuzi.

Akiongea kwa njia ya simu na Mtanzania Digital kutoka Wilayani Maswa ambako ndiko alitegemea kupigia kura, Shibuda amesema kuwa ameangaika tokea asubuhi kuwatafuta wahusika wa kuweza kutatua jambo hilo lakini imeshindikana.

“ Mpaka asubuhi hii hakuna barua ya wakala wa chama changu ambaye amepatiwa barua, wote wamekataliwa kuingia ndani ya vituo, namtafuta msimaizi wa uchaguzi hapokei simu yangu, Nimeamua kutokwenda kupiga kura mpaka pale mawakala wangu watakapopatiwa barua hizo ,” amesema Shibuda….

Mtanzania Digital imemtafuta msimamizi wa uchaguzi katika majimbo hayo Dkt. Fredrick Segamiko, ambaye amesema hana mamlaka ya kumwongelea mgombea urais.

“ Mgombea urais mamlaka ya kumwongelea ipo tume ya taifa ya uchaguzi, mimi siwezi kuongelea chochote juu yake, malalamiko hayo tume ndiyo wenye mamlaka ya kuongelea, mimi naweza kuongelea malalamiko ya wabunge au madiwani,” amesema Dkt, Segamiko.

Msimamizi huyo amesema kuwa licha ya kutokuwa na mamlaka ya kumwongelea mgombea Urais, ameeeleza malalamiko hayo hayana ukweli kwani wagombea wote wa ubunge na udiwani wakiwemo wa chama hicho hakuna aliyeleta malalamiko hayo kwake.

Amesema kuwa mawakala wote wa vyama ambao aliwaapisha, barua za utambuzi zilianza kupelekwa jana na nyingine zimepekwa leo asubuhi na zimewafikia wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles