JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

0
334

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi kutimiza ndoto za kufanya wimbo, Tena na Tena na rapa nyota nchini humo, Cannibal.

Maeba ambaye ni Mtanzania anayeishi Kenya, ameliambia ukurasa huu kuwa Cannibal ni miongoni mwa wasanii wakubwa Kenya waliomvutia hivyo kufanya naye wimbo ni jambo kubwa.

“Mimi nafanya Afro Pop na Bongo Fleva yenye vionjo vya RnB. Cannibal nimekuwa nikipenda muziki wake niliporudi Tanzania huo Kenya meneja wangu alituunganisha na tukafanya kazi hii ambayo imetoka jana na inapatikana kwenye chaneli yangu ya YouTube,” alisema JB Maeba.

Aliongeza kwa kusema: “Nilianza safari yangu mnamo 2015, niliamini ninaweza kusukuma sanaa yangu ya muziki mbele zaidi, imekuwa safari ngumu ila sasa mambo yanakwenda poa kwahiyo naomba sapoti kwa mashabiki.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here