24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

NEEMA| Viongozi wakuu China, Poland na Cuba kutembelea Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Diplomasia ya Tanzania yazidi kuimarika huku fursa mbalimbali za kimaendeleo zitokana na ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na nchi mbalimbali ulimwenguni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajia kupokea ugeni mkubwa wa viongozi kutoka nchi tatu kwa mwezi huu wa Januari pamoja na Februari lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kati ya Tanzania na mataifa mengine.

Hapo kesho Januari 22, 2024, Rais Samia anatarajia kumpokea, Liu Guozhong-Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China anayekuja nchini kwa ziara ya siku tatu.

Salvador Valdes Mesa.

Katikati ya ujio wa kiongozi huyo wa China, Januari 23, Mwaka huu Rais Samia atapata ugeni mwingine wa Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa atakayekaa nchini kwa siku tatu lengo likiwa ni kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili.

Baadhi ya mambo atakayofanya, Valdes na viongozi wengine wakubwa wa nchi, Bara na Zanzibar, kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa ya Biolarvicide cha Kibaha na kusalimiana wa Watanzania waliosoma Cuba.

Rais wa Jamhuri ya Poland, Andrzej Duda.

Rais wa Jamhuri ya Poland, Andrzej Duda anatarajia kuwa na ziara ya kikazi ya siku Februari 8 na 9, mwaka huu katika hatua ya kuimarisha Diplomasia kati ya Tanzanua na Poland ambazo zina uhusiano mzuri katika miradi ya maendeleo ya miundombinu, uhifadhi wa wanyama pori, elimu, maji na usimamizi wa mazingira, utalii, biashara na uwekezaji bila kusahau ushirikiano wa mabunge.

Mbali na viongozi hao kuja Tanzania, Rais Samia amealikwa kufanya ziara za Kitaifa nchini Indonesia, Vatican na Norway. Hii ni ishara kuwa Tanzania inazidi kufungua mipaka yake kimataifa na kuwa ina ushirikiano mzuri wa kidiplomasia na mataifa mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles