29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Budju amaliza Utukufu Concert Uganda

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Staa wa gospo nchini Canada, Jonathan Budju, amemaliza kwa kishindo tamasha lake ‘Utukufu Concert’ jijini Kampala, Uganda.

Budju anayetamba na ngoma kibao kama vile Tawala, Utukufu, Hosanna amekuwa nchini Uganda kwa muda wa mwezi mmoja akitumbuiza na kutoa misaada ya kibinadamu kupitia taasisi yake ya Jonathan Budju Foundation.

Akizungumzia ziara hiyo, Jonathan amesema imekuwa na mafanikio makubwa tofauti na matarajio yake kwani watu wamemwona Mungu kupitia nyimbo zake alizoimba kwenye tamasha la Utukufu Concert.

“Nimesharudi nchini Canada lakini mawazo yangu bado yako Afrika, kwasababu nimemuona Mungu akiwahudumia watu kwenye Utukufu Concert na mimi nimewagusa watoto waliopo kwenye mazingira magumu kupitia taasisi yangu,” amesema Jonathan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles