25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aalikwa Vatican na Papa Francis

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kufuatia mualiko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoloki duniani na nchi ya Vatican, Papa Francis, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya Kitaifa ya sku mbili Februari 11 na 12, mwaka huu nchini Vatican.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 21, 2024 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba amesema lengo la ziara hiyo ni kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Vatican.

Kwa mujibu wa Makamba, Tanzania na Vatican tangu mwaka wa 1960 zimekuwa zikishirikiana katika masuala ya elimu, afya, amani na kiroho.

“Kanisa Katoliki linakadiriwa kumiliki zaidi ya shule za chekechea 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 245, vyuo vya ufundi 110, na vyuo vikuu 5,” inaeleza taarifa iliyotolewa na wizara huku takribani taasisi za afya 473 zikiendeshwa na Kanisa Katoliki.

Tofauti za dini hazijawafanya viongozi hawa kushindwa kukaa pamoja na kujadili maslahi ya wananchi na uendelezaji wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles