24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NDUGAI: BUNGE LIPO TAYARI  KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI

  Na SARAH MOSES-DODOMA


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amesema Bunge lipo tayari kushirikiana na vyombo vya habari   kuleta uhusiano mzuri ikiwamo   kuandika habari zenye ukweli na uhakika.

Alitoa kauli hiyo Dodoma jana alipofungua Mkutano wa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Alisema kwa sasa kumeibuka sintofahamu kwa baadhi ya waandishi kuandika taarifa zinazopotosha.

Alisema   yeye kama spika yupo tayari kushirikiana na vyombo vya habari   na kupokea maombi ambayo yatamtaka kuruhusu kamati yoyote ya Bunge ihojiwe.

Ndugai alisema kumekuwa na udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya waandishi wa habari hali iliyosababisha baadhi yao kuhojiwa na Bunge kutokana na taarifa walizoandika.

Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha kutokea   misuguano baina ya Bunge na wanahabari.

“Kwa sasa eneo la habari limekuwa la kughushi,   ndiyo maana hata wabunge wamekuwa wakiliongelea,” alisema Ndugai.

Vilevile,  alizungumzia   mitandao ya  jamii ambayo hutoa fursa kwa kila mtu kuweza kuandika kile anachokitaka bila kujali kitaathiri jamii kwa kiasi gani.

“Siku hizi kila mtu amekuwa mwandishi wa habari kwenye mitandao tena habari zenyewe ambazo hazina ukweli wowote, hivyo basi katika hili mnatakiwa kuliangalia kwa namna yake,” alisema Spika Ndugai.

Alisema kama waandishi wa habari watafanya kazi kwa weledi watasaidia mapambano ya kufichua rushwa na ufisadi  nchini.

Makamu wa Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC),  Jane Mihanji alisema kwa sasa kuna changamoto kubwa ya waandishi kujawa na hofu na kufanyakazi kwa pasiko uhuru huku wengi wao wakiwa na hofu ya kukamatwa na watu wasiojulikana.

“Waandishi wamekuwa na hofu katika utendaji wao wa kazi hali inayosababisha  kukosekana   uhuru wa habari,” alisema Mihanji.

Naye Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, Salome Kitomari alisema   sheria zinazotungwa na Bunge zihakikishe haziminyi uhuru wa vyombo vya habari.

“Tanzania bila waandishi haiwezi kuendelea  kwa sababu  inatutegemea katika kufikisha habari sehemu mbalimbali,” alisema Kitomari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles