24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

NAMIBIA KUCHUKUA ARDHI YA WAZUNGU

Windhoek, Namibia


RAIS wa Namibia, Hage Geingob amelalamikia kucheleweshwa   mabadiliko ya sheria za umiliki wa ardhi kwa ajili ya kuwalipa wamiliki wa kizungu fidia inayostahili.

Akihutubia taifa hilo katika maadhimisho ya   miaka 27 ya uhuru,  Geingob alisema   serikali imetumia kila mbinu kuwapa ardhi Waafrika kwa kutoa fursa kwa wale wanaouza na kununua kwa hiari.

Geingob amesema serikali itaitumia katiba ambayo inaruhusu kuchukuliwa   ardhi na kulipa fidia inayostahili.

Umiliki wa ardhi ni suala lenye utata ukanda huo na Serikali ya Zimbabwe pia imekuwa ikilaumiwa  na upinzani na mataifa ya nje kwa kuchukua ardhi iliyomilikiwa na wazungu.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ametoa wito ya kuwanyang’anya ardhi bila ya kulipa fidia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles