RAIS WA ZAMANI WA KOREA KUSINI AHOJIWA

Seoul, Korea Kusini


Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani, Park Guen-Hye amehojiwa na waendesha mashitaka kuhusu kashfa ya ufisadi iliyosababisha  atimuliwe kwenye madaraka.

Park amehojiwa baada ya kuwakwepa waendesha mashitaka kwa miezi kadhaa wakati alipokuwa madarakani.

Amewaomba radhi wananchi lakini amekanusha kufanya makosa wakati alipowasili katika ofisi za waendesha mashitaka mjini Seoul na kuahidi kushirikiana kwa ukamilifu katika uchunguzi huo.

Wafuasi wa Park walikusanyika nje ya nyumba yake katika mtaa wa kifahari mjini Seol alipokuwa akisindikizwa na polisi kwenda  ofisi za wakuu wa mashtaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here