27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mwenye kesi ya mauaji alilia ucheleweshwaji upelelezi

Na Mwandishi Wetu – SINGIDA

UPANDE wa utetezi katika kesi ya mauaji inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi Wilaya ya Manyoni, Pius Luhende (54) na wenzake, umeomba kuharakishwa   upepelezi wa shauri hilo.

Wakili wa mshatakiwa, Victoria Revocati, aliomba upande wa mashitaka uharakishe kumaliza upelelezi kwa sababu kesi hiyo haina dhamana.

Hata hivyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu  Mkazi Singida, Consolata Singano, alisema kwa sasa ni mapema mno kulalamikia ukamilikaji wa upelelezi kwa kesi ya mauaji.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni  Rodey Elias (46), Makoye Steven, Silvanus Lungwisha (50), Elick Paul (31), Eliuta Agustino (43) na Yusuph Yohana (25).

Mapema jana, Wakili wa Serikali Mkuu, Michael Ng’hoboko, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Consolata Singano, kwamba washitakiwa hao kwa pamoja, walitenda kosa hilo la kumuua mkulima, Isack Petro (28) mkazi wa Kijiji cha Kazikazi Tarafa ya Itigi, Februari 2 ndani ya kanisa.

Alidai walitenda kosa hilo katika Kata ya Kitaraka Tarafa ya Itigi.

Washitakiwa hao  saba hawakutakiwa kujibu cho chote kwa vile mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 11.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,549FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles