23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

Soko la dhahabu Geita kuanza karibuni

NA  HARRIETH MANDARI- GEITA

SOKO kuu la dhahabu mkoani Geita linatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni, imefahamika.

Katibu wa Kamati ya  Uanzishaji   Masoko ya Madini ikiweamo dhahabu mkoani Geita, Ramadhani Mcharo amesema ujenzi wa soko hilo  uko katika hatua za mwisho baada ya kukamilika kwa asilimia 85.

 Mcharo alikuwa akizungumza   katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Geita juzi.

 Awali kumekuwa na changamoto kubwa ya soko la dhahabu kiasi kwamba  wachimbaji wengi wamekuwa wakihangaika kupata sehemu ya kuuzia bidhaa yao.

Wengi wao walilazimika kuuza   nje ya nchi jambo ambalo lilikuwa   likiikoseha serikali mapato  na hata  kuleta usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara hao.

Mcharo alisema  kutakua na soko kuu mjini Geita na mengine madogo manane.

“Masoko madogo yataanzishwa katika maeneo yote yenye uchimbaji madini hali itakayosaidia  kuondokana na changamoto ya soko,”alisema.

Alitaja maeneno ya uchimbaji ambako masoko  madogo yataanzishwa kuwa ni  Nyarugusu, Nyakagwe, Rwamgasa, Chato, Bukombe, Ushirombo  na Masumbwe.

Alisema katika soko kuu kutakua na vyumba 14 kwa ajili ya wanunuzi wa dhahabu, ambavyo tayari vimekwisha kupata wanunuzi.

 Mcharo alisema    leseni za wanunuzi zipatazo saba zimekwisha kukamilika usajili na nyingine sita ziko katika hatua ya mwisho ya usajili.

Pia alisema wapo madalali wa dhahabu wapatao 114.

Ofisa Madini wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda alisema kuwapo  masoko hayo ya madini kutasaidia kuongezeka   mapato ya serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,  Robert Gabriel alitoa rai kwa watendaji kuhakikisha fedha zinazopatikana zinatumika  vizuri  kwa kuzipa kipaumbele  sekta muhimu kama afya na elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles