26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mwangozo wa jua haki yako, linda ardhi ya mwanamke wazinduliwa Kilimanjaro

Na Clara Matimo, Kilimanjaro

Wakati  Tanzania jana  ikiwa imeungana na nchi zingine duniani kusherekea maadhimisho ya siku ya mwanamke anayeishi kijijini  yanayoadhimishwa Oktoba 15, kila mwaka wanawake hao wamekutana Mkoani Kilimanjaro kwenye kongamano la taifa la haki za wanawake katika ardhi na kuzindua kitabu chenye mwongozo wa ‘jua haki yako linda ardhi ya mwanamke’.

Mwongozo huo umezinduliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wanaojishughulisha kutetea haki ya mwanamke katika kumiliki ardhi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya ‘linda ardhi ya mwanamke’ ambayo inatekelezwa kimataifa na nchi mbalimbali ikiwemo Uganda na Ethiopia inayolenga kulinda haki ya mwanamke katika kumiliki ardhi.

Akizungungumza baada ya kuzindua mwongozo huo, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Grace Mwangwa,aliyemwakilisha Waziri wa Wizara hiyo Dk. Doroth Gwajima, amesema utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake katika kumiliki ardhi maana unatoa fursa kwa wanawake kuelewa sheria mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi.

Kampeni hiyo inatekelezwa na mashirika 25 yanayotetea haki  ya mwanamke katika kumiliki ardhi na inaratibiwa na Shirika linalojishughulisha na masuala ya ardhi la Landesa  kwa kuongozwa na  Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania( TAWLA).

Mkurugenzi wa landesa, Dk. Monica Mhoja, amesema mwongozo huo pamoja na kampeni italeta mabadiliko chanya katika jamii  kwa mwanamke kumiliki ardhi kwa sababu wamefafanua vipengele vyote vya sheria inayohusu masuala ya ardhi na haki za umiliki wa rasilimali hiyo kwa lugha nyepesi.

“Lengo la mwongozo huu ni kuwasaidia wanachama na wadau wote wanaolinda ardhi ya mwanamke, unazungumzia sheria  mbalimbali zinazohusu  ardhi  kama sheria zinazogusa muda wa usajili wa ardhi na ukomo wa kuleta mashtaka kwa suala la ardhi ambapo vipengele mbalimbali vya sheria tumeviweka sehemu moja tena kwa lugha nyepesi kabisa  kwa hiyo inakuwa rahisi kwa kila mtu kusoma na kuelewa hata kama si mwanasheria.

“Tanzania tunakila sababu ya kujivunia kampeni hii ambayo tulianza kuitekeleza mwaka 2019 yenye lengo la kujaribu kuziba ufa uliopo kusaidia wadau kujua sheria  maana tumeteuliwa kimataifa kuwa nchi ya mfano katika kuitekeleza kutokana na kuwa na sheria nzuri lakini utekelezaji wake ni hafifu hii inatokana na watanzania wengi kukosa elimu ya sheria moja ya sababu ikiwa ni sheria hizo kuandikwa kwenye vitabu vikubwa,”amesema.

Ametoa wito kwa wanawake kuhamasika kuomba  kumiliki ardhi pia wahudhurie mikutano ya kijiji ili washiriki kutoa maamuzi huku akiwasisitiza kushiriki   katika vyombo vya maamuzi yanayohusu masuala ya ardhi ambapo amebainisha  kwamba ardhi ni nyenzo muhimu katika ustawi wa maisha ya mwanamke na familia kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Shirika la We Effect kanda ya Afrika Mashariki, George Onyango, ambalo limefadhili maadhimisho hayo na kuratibiwa na TAWLA  akizungumza na washiriki wa kongamano hilo kwa njia ya mtandao akiwa jijini Nairobi nchini Kenya amesema wataendelea kusaidia Tanzania  katika masuala yanayohusu ardhi.

“Hadi sasa  tunafanya kazi na mashirika 12 huko Tanzania tumeweka jitihada  kwenye mashirika hayo ambayo yanatetea haki za binadamu na maeneo mengine lakini naishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kusukuma na kuchochea mabadiliko katika masuala yanayohusu wanawake wanaoishi vijijini pia kupitia ajenda ya maendeleo endelevu vijijini  ambayo imekuwa ikitoa uzito mkubwa,”amesema Onyango.

Kongamano hilo lilikutanisha wanawake wanaoishi vijijini kutoka mikoa ya  Mwanza, Shinyanga, kilimanjaro, Njombe, Arusha, Manyara, Pwani, Tabora, Tanga, Singida  Dar es Salaam, Mbeya

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles