23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Kitila awaalika wafanyabiashara, sekta binafsi maonesho ya Expo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo, amewaalika wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara kushiriki maonesho ya dunia ya Expo 2020 Dubai ambayo yameanza mwezi huu hadi Machi 31 mwakani.

EXPO ni maonesho ya dunia yanayosimamiwa na Shirika la Kimataifa lijulikanalo kama Bureau of International Exhabition (BIE) lenye nchi wanachama 195.

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Khamis.

Amesema mwaka 2013 nchi za Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) zilichaguliwa kuwa wenyeji wa EXPO 2020 Dubai na maonesho hayo yalipangwa kufanyika kuanzia Oktoba Mosi 2020 hadi Machi 31, 2021 lakini kutokana na changamoto ya ugonjwa wa UVIKO 19 yalisogezwa mbele.

Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 191 ambazo zinashiriki maonesho hayo yaliyoanza mwezi huu yakitarajiwa kumalizika mwakani Machi 31 na kwamba yanaratibiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade).

Amesema kutokana na changamoto ya UVIKO 19 waandaaji wa EXPO 2020 Dubai wanahamasisha wafanyabiashara duniani kote kutumia fursa ya soko mtandao ambao hauna tofauti na mitandao maarufu duniani.

“Nawaalika wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara kushiriki maonesho ya dunia ya Expo 2020 Dubai kupitia programu mbalimbali ambazo zimeandaliwa ikiwemo ziara za kujifunza na mikutano ya kibiashara (B2B),” amesema Profesa Mkumbo.

Waziri huyo amesema programu hizo zinajikita katika teknolojia, mipango miji na vijiji, elimu, ufundi na ubunifu, mifumo ya ufundishaji, fursa za utalii, michezo, mazingira na fukwe, usafirishaji na mawasiliano, kilimo uongezaji thamani wa mazao.

Amesema waonesho hayo hufanyika kila baada ya miaka mitano ambapo hudumu kwa miezi sita yakiwa na kaulimbiu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa nchi washiriki.

Kwa mujibu wa Profesa Mkumbo, Tanzania inatangaza miradi ya kimkakati kama vile mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), reli ya kisasa (SGR) upanuzi wa Bandari ya Dar es salaam, ujenzi wa viwanja vya ndege na kuimarisha usafiri wa anga.

“Nchi yetu inatarajia kutumia fursa hii kubwa kushirikiana na sekta binafsi kutangaza na kutafuta mnasoko ya uhakika na endelevu ya bidhaa zinazotokana na mazao ya kimkakati kama vile kahawa korosho, chai, mkonge, karafuu, viungo, bidhaa za ngozi pamoja na bidhaa nyingine zinazokidhi mahitaji ya soko la kimataifa,” amesema.

Aidha amesema manufaa ya kushiriki maonesho hayo ni makubwa ikiwemo kuvutia na kushawishi upatikanaji wa mitaji katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kupata wabia wa uwekezaji watakaoendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi.

Amesema maonesho hayo yatatoa fursa kwa makampuni kujitangaza na kunadi bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini ili kupata masoko ya uhakika kimataifa.

Naye Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Khamis, amesema; “Tunawakaribisha Watanzania wote kushiriki maonesho haya makubwa yanayofanyika kila baada ya miaka mitano. Ni maonesho makubwa zaidi duniani nchi 191 zinashiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles