23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanajeshi akamatwa na mirungi

Beatrice Mosses, Manyara

Jeshi la Polisi mkoani Manyara, linamshikilia Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Monduli mkoani Arusha kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 20.

Akithibitisha kukamatwa kwa askari huyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Augustino Senga amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Novemba jana saa 16:50 jioni maeneo ya Minjingu Kata ya Nkaiti, Wilaya ya Babati wakati askari wakiwa katika upekuzi wa magari na ufuatiliaji wa taarifa fiche.

“Wakati wanaisimamisha gari lenye namba T543DHJ, aina ya Alteza ikitokea Makuyuni, Arusha katika kizuizi cha mabasi Minjingu, ghafla gari hilo lilibadilisha mwelekeo kurudi nyuma kuelekea Arusha na ndipo askari hao walipotilia shaka na kuanza kuifukuza kwa nyuma na kufanikiwa kuikamata maeneo ya Nanja Wilaya ya Monduli ikiwa inaendeshwa na dereva mwanajeshi mwenye namba  MT. 12014 Abdul Bashiri Ally miaka 25 Askari wa JWTZ Monduli Arusha,”amesema Kamanda Senga.

Kamanda Senga amesema baada ya kuipekua gari hiyo ilikutwa ba bunda 60 za mirungi sawa na kilo 20 ikiwa imehifadhiwa kwenye buti la gari hilo.

“Mtuhumiwa amekamtwa kwa mahojiano kubaini mahali alikoitoa na kubaini mtandao wake kwani wakati anakamatwa mwenzake alishuka kwenye gari na kutoroka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles