Waziri wa Kilimo awasili Mtwara kuhakiki Korosho

0
1373
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi

Mathias Canal, Wizara ya Kilimo, MtwaraWaziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amewasili mkoani Mtwara kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu yaliyopo katika mikoa ya kusini ikiwamo Mtwara na Lindi.

Hasunga katika ziara hiyo ameambatana na viongozi wakuu wa Wizara yake akiwamo Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa na Katibu Mkuu, Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Siza Tumbo.

Viongozi hao wakuu watahakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa unasimamiwa na Bodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala na Usimamizi wa ziada wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.

Aidha, viongozi hao watahakiki kiasi cha Korosho kwenye ghala kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya Korosho kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo kwenye taarifa za stakabadhi ya ghala (Warehouse Report).

Hasunga amechukua hatua hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya kuapishwa kuongoza wizara hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here