32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

TRA: Udhibiti magendo bandari bubu umewabana wakwepa kodi

Susan Uhinga, Tanga


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga, imesema kuundwa kwa timu ya kudhibiti uingiaji wa magendo mkoani humo kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuwabana wakwepa kodi wanaotumia bandari bubu kuingiza bidhaa badala ya kutumia bandari zilizowekwa kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na meneja wa TRA mkoa wa Tanga, Massawa Masatu, wakati wa ufunguzi wa warsha ya kodi iliyoandaliwa na mamlaka hiyo kwa wanahabari wa Mkoa wa Tanga.

Masatu amesema suala la kodi linatakiwa kuwepo kwa nguvu ya pamoja kati ya maofisa wa TRA, wadau wa kodi na wananchi.

Amesema kamati hiyo imeundwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, ikiwa imewajumuisha watendaji mbalimbali kutoka katika taasisi za serikali ikiwemo Mamlaka ya Bandari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirila la Viwango mchini (TBS) na taasisi nyingine.

Awali akifungua warsha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobiasi Mwilapwa, amewataka waandishi wa habari mkoani hapa kushiriki kikamilifu katika kuhabarisha wananchi kuhusu swala la ubaya wa biashara za magendo zinazooitishwa katika bandari bubu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles