24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi IFM adaiwa kufanya shambulio la aibu

NA MANENO SELANYIKA, DAR ES SALAAM

MWANAFUNZI wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mussa Msafiri (23), alipandishwa kizimbani   katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jana akituhumiwa kumwingizia vidole sehemu za siri mtoto (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka minne.

Mbele ya Hakimu Issa Kasailo, Wakili wa Serikali, Matarasa Maharagande, alidai  mtuhumiwa alitenda kosa hilo   Januari 7 mwaka huu maeneo ya Sinza alikokuwa anaishi mwanafunzi huyo.

“Mtuhumiwa ulitenda kosa hilo wakati ukitambua kwamba ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai wakili.
Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na upelelezi  unaendelea.

Hakimu Kasailo alisema   shtaka hilo linadhaminika hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaoweka saini ya maandishi ya Sh milioni tano kwa kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Febuari 27 mwaka huu na mtuhumiwa aliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

Wakati huohuo, Mwalimu wa kujitegemea wa Shule ya Tumaini Nursary School iliyopo Kibamba Hospitali, Rose John (46), amefikishwa  katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumjeruhi kichwani mwanafunzi Samwel Isaya kwa kipande cha tofali.

Mbele ya Hakimu Obadia Bwegoge, wakili wa Serikali, Nancy Mushumbusi, alidai   mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 27, mwaka jana eneo la Kibamba Hospitali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles