31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Twiga wa ajabu aonekana Tanzania

Joseph Hiza na Mashirika

TWIGA mwangavu aliyepewa jina la Omo ameonekana akivinjari katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire wilayani Monduli mkoani Arusha   akiwa na kundi la wenzake ambalo halikuonekana kumshangaa kutokana na kutofautiana nao.

Mwanajiolojia Dk. Derek Lee, mwanzilishi na mwanasayansi katika Taasisi ya Mazingira Asili, ndiye aliyembaini twiga huyo mwang’avu.

Derek(45), alisema: ‘Hali ya Omo kwa kitaalamu hujulikana kama ‘leucistic’, akimanisha sehemu kubwa ya seli za ngozi yake hazina uwezo wa kutengeneza   rangi lakini baadhi zina uwezo huo na   ndiyo maana yu mwangavu   na macho mekundu au bluu kama walivyo binadamu albino.

“Hata hivyo twiga huyo si albino, bali kama tulivyoona ni leucism, ambayo licha ya kuchangia macho mekundu au bluu kama albino, huwa na ngozi nyeupe angavu wakati albino ni weupe kamili.

“Hii ni hali ya kinasaba,” ‘Omo ni twiga pekee mweupe ambaye hadi sasa tunamfahamu, lakini tumewahi kuona wanyama wenye hali kama yake wakiwamo kongoni, nyati na mbuni katika Hifadhi ya Tarangire’.

Aliongeza: ‘Omo anaonekana kuzoeana na twiga wengine, daima amekuwa akionekana akiwa na kundi kubwa la twiga wa rangi ya kawaida ambalo halionekani kujali utofauti wake wa rangi.

‘Omo kwa sasa ana umri wa miezi 15, akiwa amefanikiwa kupita mwaka wake wa kwanza kama twiga mtoto kipindi ambacho ni hatari zaidi kwa twiga wadogo kutokana kuwindwa mno na wanyama wakali wala nyama kama vile simba, chui na fisi.

‘Fursa yake ya kuendelea kuishi   ni kubwa lakini twiga wakubwa mara kwa mara hukumbana na ujangili unaolenga nyama ya pori na rangi yake ya ajabu inaweza kuwa kivutio zaidi kwa majangili.

“Sisi na washirika wetu tunafanya kazi kwa ajili ya uhifadhi wa twiga na shughuli za kupinga vitendo vya ujangili, ambazo zitamsaidia Omo na wenzake fursa nzuri ya kuishi miaka mingi ya kawaida.

‘Tuna matumaini ataishi  maisha marefu na siku moja atazaa watoto wake.’ Taasisi hiyo inafanya utafiti wa sayansi kutoa elimu kwa umma na harakati za ushawishi juu ya kutunza uasili.

Inaendesha mradi mkubwa zaidi kuwahi kufanywa wa utafiti wa twiga, kutambua kila twiga aliyepo na kuandika ripoti ya maisha ya twiga zaidi ya 2,100 wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles