30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge afukuzwa kikaoni

Na Asifiwe George, Dar es Salaam

SINTOFAHAMU kubwa imeghubika  uchaguzi wa  kumpata  mwenyekiti  na makamu  wa Halmashauri ya Wilaya  ya Kilombero baada ya kuzuka vurugu kubwa na kusababisha uchaguzi huo kutofanyika.

Katika vurugu hizo, Mbunge wa Kilombero, Ambrose Elijualikali aliambiwa si mjumbe halali wa mkutano huo jambo ambalo lilipingwa na kuzua vurugu na kuwalazimu  polisi kuingilia kati kumtoa kwa nguvu ukumbini.

Hali hiyo ilitokana na kile kilichodaiwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitaka kuingiza wajumbe ‘mamluki’ ambao ni wabunge wa viti maalum kutoka Singida na Tabora.

Hatua hiyo ilionekana kama  kuongeza idadi na kuwazidi madiwani wanaotokna na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).  Idadi ya wajumbe halali wa Ukawa ni 19 na CCM 18.

Habari kutoka Kilombero zilidai kuwa, awali wajumbe halali wa CCM walisusa kwa muda kuingia katika kikao na baadaye waliingia wakiwa pamoja na nyongeza ya wajumbe wawili ambao ni Asha Matembe (Viti maalum Tabora)    na Fatuma Patrick (Singida).

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga alisema baada ya kuona wenzao CCM wameingiza mamluki walimshauri mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutumia kanuni iliyotumika katika halmashauri za Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam lakini aligoma na kutaka kulazimisha wabunge hao kushiriki katika uchaguzi huo.

“Mbunge halali wa Kilombero amedhalilishwa akiambiwa hapaswi kupiga kura si diwani… ni aibu mkurugenzi kushindwa kuongozwa na sheria ili kuwabeba CCM.

“Katika hili hatutakubali kuporwa haki yetu ya kuunda halmashauri itakayoongozwa na Ukawa,” alisema Suzan ambaye pia ni mbunge wa Mlimba (Chadema).

Wakati wabunge hao wa CCM wakikataliwa kupiga kura  msimamizi wa uchaguzi aliwakataa wabunge wa Chadema, Devota Minja, Kunti  Majala na Mbunge wa Kilombero, Lijuakali kwamba si wapiga kura halali katika kikao hicho cha uchaguzi.

Wakati huo huo Uchaguzi wa Mji mdogo wa Ifakara umekamilika ambako Mashaka Mbilinyi alichaguliwa kuwa  mwenyekiti na makamu ni Sambo Maganga, wote kutoka Chadema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles